UJIO WA VIDEO YA MAUA KUTOKA KWA MWIMBAJI BEATRICE KITAULI. HABARI PICHA HIZI HAPA



Kutoka Tanzania Mwimbaji Beatrice Kitauli amefunguka rasmi kuhusu ujio wa video yake mpya inayotambulika kwa jina la MAUA ambayo anatarajia kuiachia siku chache zijazo akiongea na GospoMedia mwimbaji Beatrice Kitauli amesema kuwa kwasasa yupo kwenye mchakato wa kumalizia video hiyo ambayo ana hakika itakwenda kuwabariki watu wengi kutokana na ubora wa video yenyewe ambayo inaongozwa na kutengenezwa na director Msafiri Shabani na Eric Mlindiwa kutoka kampuni ya Kwetu Studio, Hata hivyo Beatrice amesisitiza kuwa kwasasa ameamua kuwa makini sana katika kuandaa kazi zake kwakuwa anapenda kufanya kazi zenye ubora zaidi kwakuwa hata Mungu anataka kuona kazi za Muziki wa Injili zikiwa kwenye kiwango cha hali juu katika kulitukuza Jina lake kupitia Uimbaji na hivyo amewaasa pia waimbaji wenzake kuwa wasipende kufanya kazi zao ilimradi(Bora liende) hii inashusha ubora wa tasnia ya Muziki wa Injili Tanzania kwakuwa muziki huu sasa unahitaji kuvuka mipaka na kufika kila pande ya dunia hii katika kuitangaza Injili ya kweli kwa watu wote, pia Beatrice amewaomba wadau na mashabiki wake wote kumwombea na kukaa tayari kupokea video ya wimbo wake mpya ya MAUA ambayo anaamini itakwenda kumbariki na kumwinua kila mtu kiroho. GospoMedia leo tumekuletea baadhi ya picha za maandalizi wa video hii ya MAUA ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni. endelea kutembelea tovuti ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kuitazama. Barikiwa sana!!


Mwimbaji Beatrice Kitauli na director Msafiri wakishoot video ya wimbo wa Maua.




Mwimbaji Beatrice Kitauli akiimba wakati anashoot video ya wimbo wake mpya Maua.


Beatrice kitauli akiwa na madancer wake wakishoot wimbo wa Maua.


Mwimbaji Beatrice Kitauli akicheza pamoja na madancer wake.


Mwimbaji Beatrice Kitauli akiwa katika Pozi.


Mwimbaji Beatrice Kitauli akicheza wimbo wa Maua wakati anashoot video yake.

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Beatrice kitauli kupitia
WhatsApp: +255757830451
Facebook: Beatrice Kitauli
Instagram: beatrice_Kitauli
YouTube: Beatrice Kitauli
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment