HIVI NDIVYO DIRECTOR JACKSON JOACHIM ALIVYOJIPANGA KUZIPELEKA VIDEOS ZA GOSPO KIMATAIFA ZAIDI.








Siku hizi kwenye uwanja wa Gospo watu hawapumui..harakati za kusaka vitu bora zinaendelea siku baada ya siku kiasi cha kwamba waimbaji wengi wenye uwezo kwa sasa wamekua wakivuka mipaka ya Tanzania kwenda kusaka kinachoitwa Ubora.
Lakini Je hakuna jambo jema linaloweza kutoka Tanzania? Video bora haziwezi kufanyika Tanzania?.Siku za hivi karibuni nimekutana na muongazaji wa video kutoka hapa nyumbani kwetu Tanzania ambaye kasi yake imekuwa kubwa sana kwenye upande wa kufanya video za Gospo naye si mwingine ni Director Jackson Joachim kutoka Blessing Studios.

Jackson amefanya video kadhaa za gospo na zisizo za gospo unaweza kuzitazama hapa. cha kwanza nilichotaka kujua kutoka kwake ni mwelekeo mzima wa tasnia ya video kwa upande wa muziki wa gospo ambapo director huyo ameweka wazi kuwa tasnia ya video kwenye gospo inaelekea pazuri tofauti na zamani ambapo watu walikuwa hawazingatii utaalamu na ubora zaidi.
Licha ya mwelekeo mzuri wa tasnia ya video za Gospo hapa Tanzania waimbaji wengi wamekua wakienda na wengine kutamani kwenda kufanya video nje ya nchi hususani Kenya, ambapo Director huyo alidai kuwa watu wanaona video za Kenya zinakuwa nzuri kwa sababu waimbaji wa huko wanatoa bajeti nzuri kwa ma-director ili wafanye kazi nzuri.
Unajua waimbaji wengi wa Tanzania wanataka wa shoot album nzima kwa bajeti ya milioni moja, Wakenya wenzetu wako tayari kufanya video moja hata kwa milion tano, Niliwahi kuchat na J blessing, yeye anafanya video moja kwa milioni nne. Watanzania ni ngumu kuwafikia wale kwa sababu wale wanapohitaji bajeti kufanya video nzuri wanapata. Ukimwambia mteja inabidi utoe kiasi fulani , tufanye set fulani ili kitokee kitu fulani kizuri anakuwa hakuelewi , mwisho wa siku mnaenda ku shoot kwenye maua, chini ya miti na sehemu finyu” alifunguka Director Joachim.
Kuondokana na tatizo hilo Director Jackson Joachim amesisitiza kuwa inahitajika elimu kwa waimbaji wa Tanzania akidai watu wengi mawazo yao yako Tanzania pekee, wakati kwa sasa muziki wa Injili wa Tanzania unatazamwa duniani kote kutokana na kukua kwa teknolojia ya utandawazi.jackson joachim 1
Nilipotaka kufahamu kwa upande wake amejipangaje ili kuweza kutatua matatizo ya ubora yanayoikabili tasnia ya video kwenye muziki wa Injili , Jackson amefunguka kwamba yeye kama Director cha kwanza amewekeza kwenye kazi yake ikiwemo kupata vifaa stahiki vyenye ubora wa hali ya juu pamoja na kuwekeza kwenye ujuzi zaidi.
Mimi kama Director nimejipanga kwa kuwekeza kwenye vifaa, kwa sasa natumia camera yenye ubora wa juu kabisa yaani 4k, Pia natumia teknolojia ya drones (helicopter ndogo za ku-shoot video) na vifaa vingine vya muhimu lakini pia najiongeza kwenye ubunifu kila siku kuhakikisha sifanyi video za kawaida kawaida” alisema director Jackson Joachimambaye kwa sasa yupo kwenye harakati za ku-shoot album mpya ya Beatrice Mwaipaja.
Unaweza kutazama kionjo cha video ya wimbo mpya wa Beatrice Mwaipaja hapa chini, video ikiwa imefanya na director Jackson Joachim.Pia unaweza kuwasiliana na Director Jackson Joachim kwa namba 0712343938
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment